Baraza Kuu CHADEMA kutoa mwelekeo wa chama

0
231

Baraza Kuu la chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) linafanya kikao chake mkoani Dar es Salaam, ambapo ajenda tano zinatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa.

Kikao hicho kinahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 400 wa CHADEMA kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA John Mrema amesema miongoni mwa ajenda zitakazowasilishwa na kujadiliwa katika kikao hicho cha Baraza Kuu la CHADEMA ni mpango mkakati wa chama kwa miaka mitano na mpango kazi wa mwaka mmoja.

Ajenda nyingine ni rufaa ya nidhamu iliyokatwa na wabunge 19 wa viti maalumu wakipinga kuvuliwa uanachama na Kamati Kuu ya CHADEMA iliyokutana mwishoni mwa mwaka 2020.

Habari zaidi zinaeleza kuwa Wabunge hao wakiongozwa na Halima Mdee nao wapo katika kikao hicho cha Baraza Kuu la CHADEMA.