Hoyce Temu amtembelea Balozi wa Kenya Geneva

0
204

Balozi na Naibu Mwakilishi waTanzania katika Umoja wa Mataifa (UN),Hoyce Temu leo tarehe 10/05/2022 amemtembelea Balozi na Naibu mwakilishi wa Jamhuri ya Kenya Geneva, Uswis Lucy Kiruthu.

Lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha na kuzungumzia masuala ya Uwakilishi katika Mashirika ya Kimataifa na Ushirikiano wao katika kutekeleza majukumu ya nchi zao kwa pamoja.

Pia alimkabidhi Kahawa iliyotengenezwa Tanzania toka Chama Kikuu cha Ushirika cha Kilimanjaro (KNCU) kilichopo Wilayani Moshi Tanzania.