Spika wa bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson ametoa wito kwa Wabunge kutodharau na kutweza michango ya Wabunge wenzao wanaoutoa bungeni na kusisitiza Wabunge wote waheshimiane na kama Mbunge hakubaliani na mchango wa mwenzake aseme ndani ya Bunge kwa kutoa taarifa kutokana na kanuni zinavyowaruhusu na haiiruhusiwi kutoka nje na kwenda kutweza mchango wa Mbunge mwingine.
Dkt. Tulia ametoa onyo hilo baada ya Mbunge wa Viti Maalum Dkt.Tea Ntala kuomba mwongozo wa Spika kuhusu kauli ya Mbunge wa Sengerema Hamisi Tabasamu aliyoitoa May 9, 2022 kwenye vyombo vya habari ikidaiwa amemdhihaki na kumshambulia Mbunge wa jimbo la Momba Condester Sichwale aliyekuwa bungeni na chupa za pombe akiiomba Serikali kurasimisha pombe za kienyeji ili ziwasaidie Wananchi kuwainua kiuchumi.