Nape: Tumieni anwani za makazi kutoa huduma

0
302

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Nape Nnauye amewataka watendaji wote kuanza kutumia namba za anuani za makazi katika utoaji wa huduza kwa maendeleo ya taifa.

Waziri Nape ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mzungumzo na wazee wa wilaya ya korogwe na kuwataka watendaji kuendelea kuandikisha wananchi walio salia kwani zoezi hilo halitamwacha mtu wala nyumba yoyote.

Pia waziri Nape ameupongeza Mkoa wa Tanga na watendaji wake kuweza kufanikisha zoezi hili hasa katika wilaya ambazo zilikuwa zimeshika nafasi ya mwisho katika kufanikisha zoezi hili la anuani za makazi