Mbunge wa Momba (CCM) Condester Sichalwe, ameishauri Serikali, kutafuta namna bora ya kuboresha viwango vya pombe za kienyeji ili kuzipa viwango stahiki kutokana na viwango vya TBS.
Condester ameyasema hayo Bungeni wakati wa kujadili hoja za Serikali za Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
Pia Condester ameishauri Serikali kuwa wafanyabiashara wa pombe za kienyeji wahitaji ujuzi ambao utawawezesha ubora kwa kuunda bodi ya kuwasimamia na kufanya utafiti wa kisasa.