Rais Samia aweka rekodi Uhuru wa Vyombo vya Habari

0
513

Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa Rais wa kwanza nchini kushiriki maaadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

Mwenyekiti wa Jukwaa laa Wahariri Tanzania (TEF), Deodastus Balile amesema ushiriki wa Rais katika siku hii ambayo ni Sikukuu ya Eid El-Fitr umedhihirisha dhamira yake ya kuimarisha uhusiano na vyombo vya habari.

Kidunia maadhimisho haya yanafanyika nchini Uruguay na Afrika yanafanyi jijini Arusha, Tanzania, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika nchini.

Maadhimisho haya ambayo kilele chake ni leo yalianza Mei Mosi 2022 yakitanguliwa na mijadala kuhusu sekta ya habari pamoja na maonesho ya bidhaa za tafiti zinazofanywa na taasisi zinazohusika na sekta ya habari.