Rais Samia: Royal Tour italipa hasara niliyosababisha

0
328

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa alitumia siku nane nje ya ofisi, bila kuwahudumia Watanzania,  ili kuandaa filamu ya Tanzania: The Royal Tour.

Amesema hayo katika uzinduzi wa filamu hiyo jijini Arusha, na kusema anaamini hasara aliyoisababisha kwa kutohudumia wananchi, zitalipwa na faida itakayotokana na matokeo ya filamu hiyo.

Ameomgeza kuwa katika siku hizo, ilimlazimu kuuweka urais pembeni na kufuata maelekezo ya wataalamu, hata alipotakiwa kurekodi kipande kimoja zaidi ya mara moja.