Mbunge Ndyamkama afariki dunia

0
341

Mbunge wa viti Maalum (CCM) mkoa wa Rukwa Irene Ndyamkama amefariki dunia katika hospitali ya Tumbi mkoani Pwani alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson imethibitisha kufariki dunia kwa Mbunge huyo na kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huo.