Watanzania watakiwa kuenzi na kuilinda Amani

0
491

Wakristo nchini wametakiwa kutumia Sikuu ya Pasaka kuhubiri Amani na Upendo ili kuendelea kulinda tunu hizo ambazo ziliasisiwa na viongozi wakuu wa kitaifa akiwepo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Askofu Mteule wa Kanisa la Moravian Tanzania, Lawi Mwankuga ameyasema hayo wakati wa Ibada ya Pasaka Kitaifa iliyofanyika katika Kanisa hilo Jimbo la Mashariki Ushirika wa Morogoro mjini ambapo amesema tunu za kitaifa ni lazima zilindwe ili ziweze kujenga mshikamano kwa Watanzania.

Aidha Askofu Mwankuga amesema Kupitia ufufuo wa Yesu Kristo irejeshwe heshima kwa waliodharauliwa, kutembea na kuishi kwa uaminifu, kutunza Amani, ukweli, kuwa wathubutu na wawajibikaji kwenye maisha ya kila siku.

Kuhusiana na zoezi la Sensa ya Wat una Makazi linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu, Askofu Mwankunga amesema, ni wajibu wa kila Mtanzania kujitokeza ili kusaidia Serikali kupata takwimu halisi za idadi ya Watanzania na makazi itakayosaidia kupanga mipango yake na Bajeti ya Serikali Katika kuwatumikia kwa usahihi