Mamlaka ya mawasiliano Tanzania Tcra nyanda za juu kusini imewataka wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini kufanya kazi hizo kwa kuzingatia sheria na weledi katika kutoa habari kwa jamii.
Wito huo umetolewa Mjini Mbeya na mkuu wa Tcra kanda ya nyanda za juu kusini, mhandisi Asajile John mara baada ya kukutana na wamiliki wa mitandao hiyo mkoani Mbeya.
Ameeleza kuwa mafunzo haya ni sehemu ya kuwakumbusha wadau hao juu ya sheria na taratibu za Tcra katika kutimiza majukumu yao.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Kukaja ambao ndio wasimamizi wa mitandao hiyo anawataka vijana kutumia mawasiliano ya mitandao kwa njia iliyo sahihi.