Mbunge wa Mvumi Livingstone Lusinde amsema kusiwepo na siasa kwenye suala la mfumuko wa bei na badala yake ameshauri Serikali itumie njia sahihi ya kushughulikia suala hilo.
Lusinde amesema Wananchi wengi hasa wa maeneo ya vijijini kwa sasa wanatumia usafiri wa pikipiki maarufu Bodaboda, ambapo kwa sasa lita moja ya mafuta wananunua hadi shilingi elfu nne, jambo ambalo linawaumiza wengi.
Pia ameshauri Serikali iwe na hifadhi kubwa ya mafuta ili bei ya mafuta inapopanda isilete adha kwa Wananchi.
Mbunge huyo wa Mvumi ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma alipokua akichangia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kuomba Bunge kupokea na kupitisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.