Chongolo:Jitokezeni kugombea Uongozi

0
240

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewahimiza makada na wanachama wa Chama hicho kujitokeza kugombea nafasi za Uongozi zinaendana na uwezo wao.

Chongolo ameyasema hayo wakati hafla ya kumpokea makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana mkoani Dar es Salaam.

Chongolo amesema umefika wakati wa wana CCM kujitokeza kugombea nafasi wanazoona zinawatosha ili kukitumikia Chama Chao huku akisisitiza weledi ndani ya Chama.

Aidha Chongolo amesema mkutano uliofanyika hivi karibuni Jijini Dodoma umefanya marekebisho ya Katiba ya Chama hicho ili kuiwezesha CCM kusimamia kikamilifu Serikali katika kutimiza wajibu wake wa kuwatumikia watanzania kulingana na ahadi za Chama wakati wa kampeni za 2020

Amewakunbusha viongozi wa Chama hicho kuendelea kuchapa Kazi kwa juhudi na kwenda kwa Wananchi kujua na kukabiliana na changamoto gani na kuzitafutia ufumbuzi.