Rais Samia: Mwalimu alikuwa Mzalendo wa kweli

0
165

Rais Samia Suluhu Hassan amesema, jambo kubwa ambalo mwalimu aliwafundisha watanzania ni uzalendo wa kuwapenda watu wake bila kuwabagua.

Akihutubia wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kuadhimisha Miaka 100 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere , Rasi Samia amesema Mwalimu pia alilijenga Taifa katika misingi ambayo ambayo mpaka sasa inatekelezwa na kusimamiwa na serikali.

Rais amesema, Mwalimu aliamini ili nchi iwe na maendeleo inahitaji vitu vinne ambavyo ni Ardhi, Watu, Siasa Safi na Uongozi Bora ambavyo yeye mwenyewe alivisimamia na hata sasa serikali inaendelea kuvisimamia.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kusimamia na kupigana na maadui watatu ambao hata Baba wa taifa aliyaanisha wakati wa utawala wake, Maadui hao ni Maradhi, Umasikini na Ujinga.

Rais Samia amesema, mwalimu alikataa utegemezi hivyo alisistiza katika kufanya kazi na kuweka falsa ya ujamaa na kujitegemea ikiwa ni hatua ya kukabiliana na utegemezi kwa watanzania.

Mdahalo huo umeandaliwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM), na umelenga katika kuenzi falsafa za mwalimu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mwalimu ambapo Rais pia amemkabidhi Mtoto wa Baba wa Taifa Makongoro Nyerere tuzo maalum ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mwalimu.