Mashabiki elfu 60 kushuhudia Simba Vs Orlando Pirates

0
6028

Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF limekubali ombi la Klabu ya Soka ya Simba kuruhusu mashabiki elfu 60 kuingia uwanjani kushuhudia mchezo wao dhidi ya Orlando Pirates unaotarajiwa kuchezwa Aprili 17, 2022.

Mchezo huo wa robo fainali ya CAF utakuwa wa kwanza kuchezwa kwa kutumia Teknolojia ya AVR hapa nchini huku majina ya waamuzi na wasaidizi mbalimbali wakitajwa Katika mchezo huo

Watanzania waliopata nafasi ya kusimamia mchezo huo ni pamoja na afisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo kutoka Tanzania ambaye amepewa jukumu la kuwa Ofisa Habari wa mchezo huo huku Lisobine Kisongo atakuwa Daktari wa UVIKO-19 kwenye mchezo huo.