Mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba SC dhidi ya Orlando Pirates unaotarajiwa kuchezwa Aprili 17, 2022 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, waamuzi watatumia msaada wa video [Video Assistant Referee-VAR] pale itakapobidi kutumia ili kuhakikisha maamuzi yanakuwa sahihi.
Tayari orodha ya waamuzi wa mchezo huo imeshajulikana sambamba na wale watakao ongoza VAR. Orodha ya waamuzi hao ambao ni Refa wa kati Haythem Guirat kutoka Tunisia, Refa msaidizi namba moja Khalil Hassani kutoka Tunisia, msaidizi namba mbili Samuel Pwadutakam kutoka Nigeria Mwamuzi wa akiba Sadom Selmi kutoka Tunisia, msimamizi wa VAR Ahmed Elghandour wa Misri msaidizi mwingine wa VAR Youssef Wahid Youssef wa Misri
Wengine ni Cliford Ndimbo kutoka Tanzania ambaye atakuwa Ofisa Habari wa mchezo huo na Lisobine Kisongo kutoka Tanzania atakayekuwa Daktari wa UVIKO-19
Tayari kila anayehusika na mchezo huo ikiwa ni pamoja na vilabu, wameshapewa taarifa na Shirikisho la Soka Afrika CAF juu ya uwepo wa matumizi ya VAR kwenye mchezo huo ambapo VAR itatukika kwenye mechi zote za timu zilizofuzu hatua ya Robo Fainali ya michuano ya CAF.
Hii ni mara ya kwanza VAR kutumika Tanzania kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa ikielezwa kuwa Teknolojia hiyo itatumika kwenye Michezo yote ya robo fainali ya CAF