Muhimbili yapewa miezi miwili kuboresha huduma kwa wateja

0
234

Naibu Waziri wa Afya, Dkt.Godwin Mollel ametoa miezi miwli kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kujitathimini katika utoaji wa huduma bora kwa wateja.

Akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya uchangiaji wa damu salama katika Kanda ya Mashariki Dkt.Mollel ameonesha kutoridhishwa na utoaji huduma kwa wateja katika Hospitali hiyo ya taifa na kusababisha wananchi kukimbilia huduma kwenye Hospitali za binafsi.

Aidha amebainisha kuwa kutokana namna ambavyo Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya afya inayokwenda sambamba na utoaji wa vifaa vya Kisasa kwenye Hospitali ya Taifa ni vyema hatua za haraka zichukuliwe kwenye eneo la utojai wa huduma kwa wateja ili kuwajengea wananchi imani kufuata huduma za kitabibu zenye uhakika kwenye Hospitali taifa.