Wasira: Huwezi kutenganisha historia ya Nyerere na Tanzania

0
184

Mwanasiasa Mkongwe nchini Steven Wasira amesema hauwezi andika historia ya Tanzania ama Afrika bila kuihusiaha historia ya Nyerere.

Wasira ametoa kauli hiyo wakati akielezea maisha ya Mwalimu Nyerere katika kongamano la miaka 100 ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake lililoandaliwa na Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es salaam

Amesema, historia ya Tanzania haiwezi kuandikwa popote bila kumuhusisha Mwalimu na sio historia ya Tanzania pekee bali hata historia ya ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika.

Mwanasiasa huyo amesema unapozungumza Miaka 100 ya Nyerere unazungumzia historia ya ukombozi wa Tanganyika na baadae Tanzania