Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuanza kesho

0
328

Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubeir  ametangaza kuanza kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hapo kesho.

Mufti ametoa tangazo hilo mkoani Dar es Salaam alipokuwa akigawa vyakula kwa ajili ya futari kwa baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu wenye uhitaji.

Amewataka Waumini wa dini ya Kiislamu nchini kutumia Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuliombea Taifa pamoja na Viongozi wake.