Watoto sita wafa maji

0
167

Watoto sita wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka miwili na nane wamekufa maji katika matukio tofauti yaliyotokea kwenye wilaya za Uvinza, Kasulu na Buhigwe mkoani Kigoma.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma, James Manyama amesem vifo hivyo vimetokea katika kipindi cha mwezi Machi mwaka huu, na hivyo kuwataka Wazazi na Walezi mkoani humo kuwa makini katika ulinzi wa watoto wao.

Amesema kati wa watoto hao, watano wamekufa maji walipokuwa wakikgelea na na mmoja alitumbukia kwenye ndoo ya maji.