UNFPA: Wasichana ndio waathirika wakubwa wa ukosefu wa Afya ya uzazi Tanzania

0
212

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu (UNFPA) limesema kuwa ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi miongoni mwa wazazi na walezi imekuwa chanzo cha wasichana kuacha shule wakiwa na umri mdogo.

Akiongea leo mkoani Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa Mpango Salama wa kuwalinda vijana Mratibu wa mpango huo, Fatina Kiluvia amesema vijana wanaowajibu katika jamii kwa kuhakikisha wanalinda afya zao kwa mustakabali wa taifa.

“Katika kipindi cha miaka mitatu ya programu hii UNFPA imekusudia na imejikita kuwawezesha vijana katika vipaumbele vya ujenzi na maendeleo ya Taifa yaliyoainishwa na UNFPA kwenye mpango wa maendeleo awamu ya pili (UNFPA ii 2016/17-2022).”

Kwa upande wake Afisa wa Afya chini ya Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania, Esther Majani amesema vijana ndio waathirika wakubwa wa ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi umechangia vijana kupata mimba za mapema, ndoa za utotoni hali inayopekekea kuacha shule wakiwa na umri mdogo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu  Prof. Joyce Ndalichako, anatarajiwa kuzindua Mpango April 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam