Chongolo: CCM imebeba matumaini ya Watanzania

0
202

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho unaofanyika mkoani Dodoma kuwa dhamana ya maendeleo ya Tanzania ipo mikononi mwa CCM, hivyo wana jukumu la kuwatumikia kwa nguvu kubwa.

Chongolo ametoa kauli hiyo wakati akitoa maelezo kuhusu mkutano huo ambao ni maalum kwa ajili ya kupitisha mabadiliko ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2020.

Kazi nyingine itakayofanywa na mkutano huo ni kupiga kura na kupitisha jina la mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, ambapo aliyependekezwa ni aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana.