BASATA waongeza siku 1 upigaji kura TMA

0
5042

Baraza la Sanaa la Taifa BASATA limeongeza siku Moja mbele kwa wadau wa muziki nchini kupiga kura kuwachagua wasanii wanaowapenda kulingana na vipengelee (Categories) vya tuzo za muziki Tanzania 2021.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Matiko Mniko wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika hii leo Jijini Dae es salaam.

“Zoezi la upigaji kura lilitakiwa kufungwa Leo Machi 31 usiku lakini kutokana na namna wadau wanavyoendelea kujitokeza katika mchakato huu tumeona tuongeze siku Moja ili kuwapa nafasi wale ambao walibanwa na majukumu ya hapa na pale nao waweze kushiriki,”Amesema Mniko.

Wasanii mbalimbali wanatarajia kutumbuiza katika usiku wa tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa April 2 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa.