Balozi Ole Naiko afariki dunia

0
189

Balozi Emmanuel Ole Naiko amefariki dunia leo Machi 30, 2022 nyumbani kwake Bahari Beach, Dar es Salaam.

Balozi Ole Naiko ambaye alizaliwa Julai 24, 1951 amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye serikali ikiwemo Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Hadi anafikwa na umauti alikuwa Balozi wa Heshima wa Botswana.

Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani kwake Utulivu Road, Bahari Beach, Dar es salaam