Will Smith ampiga Chris Rock kwenye jukwaa la Oscar

0
3942

Mwigizaji Will Smith amempiga mchekeshaji Chris Rock kwenye jukwaa la tuzo za Oscar baada ya mchekeshaji huyo ambaye pia alikuwa mshereheshaji kumtania mke wa Smith, Jada Pinkett Smith.

Rock alitoa matamshi hayo ya utani kuhusu Jada kunyoa nywele, ndipo Smith alisimama na kupanda jukwaani na kumpiga mchekeshaji huyo akisisitiza “toa jina la mke wangu kwenye mdomo wako.”

Jada amewahi kukiri kuwa na tatizo linalofahamika kama ‘Alopecia’ ambalo husababisha kupotea kwa nywele.

Hata hivyo baadaye Smith aliomba msamaha wakati akitoa hotuba yake kufuatia kushinda Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume.

Baada ya kupigwa, Rock alibaki jukwaani amepigwa butwaa kwa sekunde kadhaa, kisha akasema usiku huo ulikuwa ni mkubwa sana kwenye historia ya televisheni.

Aidha, Polisi jijini Los Angeles wamesema wana taarifa ya kutokea kwa tukio hilo, lakini Chris Rock amekataa kufungua jalada la mashtaka dhidi ya Will Smith.