Wanafunzi Kisutu wajifunza kwa vitendo Makumbusho

0
253

Walimu, Wazazi na Wanafunzi nchini wameshauriwa kutenga muda wao vizuri ili wapate muda wa kutembelea Makumbusho za Taifa na kujipatia maarifa zaidi ya urithi wa utamaduni na maliasili.

Ushauri huo umetollewa mkoani Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Achilesi Bufure kwa Wazazi, Walimu na Wanafunzi wa shule ya sekondari Kisutu waliotembelea Makumbusho hiyo kwa lengo la Kujifunza na kuburudika kupitia programu ya Twenzetu Makumbusho.

Bufure licha ya kuupongeza uongozi wa shule ya sekondari Kisutu kwa kuitembelea Makumbusho hiyo, ametoa wito kwa Wanafunzi hasa wa kidato cha Sita kabla ya kuanza mitihani yao watembelee Makumbusho ili wajikumbushe kwa vitendo yale waliyofundishwa.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Kisutu, Chiku Mhando amesema wanatarajia ufaulu mzuri wa Wanafunzi wa shule hiyo baada ya kujifunza kupitia Makumbusho hiyo.

Mmoja wa Wazazi wa Wanafunzi.hao wa shule ya sekondari Kisutu ameeleza kufurahishwa na utaratibu wa shule hiyo ya sekondari Kisutu kufundisha kwa vitendo zaidi, kwa kuwa njia hiyo inawafanya Wanafunzi kuelewe haraka mambo mbalimbali yanayohusu nchi yao.

Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni imeanzisha utaratibu kwa Wanafunzi wa shule za sekondari na msingi kujifunza kwa vitendo masomo wanayofundishwa shuleni, na kisha Wanafunzi hao wanaenda kufundisha wengine na kuongoza wageni ndani ya Makumbusho hiyo.