BASATA yampiga ‘stop’ Steve Nyerere

0
213

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), limetoa maelekezo kwa Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT) Steve Mengere maarufu Steve Nyerere, asianze kutekeleza majukumu ya nafasi hiyo hadi hapo itakapoamuliwa na baraza.

Taarifa iliyotolewa na baraza hilo imesema baada ya kuwepo kwa mgogoro kuhusu uteuzi wa nafasi hiyo, baraza pamoja na shirikisho wamekaa pamoja ili kufahamu kiini cha mgogoro huo na kupata ufumbuzi kwa mujibu wa katiba na sheria.

BASATA imesema kwamba sasa inafanyia kazi taarifa ya shirikisho na hoja zilizotolewa na wajumbe wa kikao.