133 wahofiwa kufa kwenye ajali ya ndege

0
369


 
Ndege aina ya Boeing 737 iliyokuwa na watu 133 imeanguka katika jimbo la Guangxi nchini China.
 
Mpaka sasa haijafahamika idadi kamili ya vifo pamoja na majeruhi wa ajali hiyo, na zoezi la uokoaji linaendelea.
 
Wakati ajali hiyo inatokea ndege hiyo namba MU5735 ilikuwa katika safari zake za kawaida kutoka katika mji wa  Kunming kwenda Guangzhou.
 
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema kabla ndege hiyo haijaanguka ilionekana katika eneo hilo kwa takribani saa moja ikizunguka, na moto mkubwa umeonekana eneo ilipoanguka ndege hiyo.