Tuzo za muziki Tanzania kutolewa Machi 2022

0
3225

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa katika mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan mambo mengi yamefanyika kuinua michezo na sanaa, na kwamba kuongeza uzito katika hayo, hivi karibuni watatoa tuzo za muziki kwa wasanii waliofanya vizuri.

Dkt. Abbasi amedokeza siri hayo katika mjadala kuhusu tathmini ya mwaka mmoja wa Rais Samia uliofanyika kupitia mtandao wa Zoom ukihusisha wazungumzaji mbalimbali wakiwemo wasanii, waigizaji na viongozi wa serikali.

“Tunapozungumza hapa tupo katika hatua za mwisho kabisa kuelekea kutoa tuzo za muziki Tanzania,” amesema Dkt. Abbasi na kuongeza kwamba hatua iliyopo sasa ni kuchagua washiriki watano kwenye kila kipengele na majina yatatolewa saa chache zijazo.

Amesema kuwa tuzo hizo zitatolewa mwishoni mwa mwezi Machi 2022, ikiwa ni baada ya miaka mingi ya kukosekana kwa tuzo hizo.

Katika tathmini yake, Dkt. Abbasi amesema Rais Samia mefanya mageuzi makubwa kwenye sekta za sanaa, utamaduni na michezo ambayo yanamanufaa makubwa kwa sekta zenyewe na Watanzania.