Watanzania wakumbuka mwaka mmoja kifo cha JPM

0
358

Watanzania leo wanakumbuka mwaka mmoja tangu kufariki dunia kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli.

Dkt. Magufuli alifariki dunia tarehe 17 mwezi Machi mwaka 2021 katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Katika kukumbuka mwaka mmoja tangu kutokea kifo cha Dkt. John Magufuli, leo, Rais Samia Suluhu Hassan anawaongoza Watanzania kwenye kumbukizi maalum itakayofanyika kwenye uwanja wa Magufuli wilayani Chato mkoani Geita.

Shughuli hiyo inayoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita , chini ya Mkuu wa Mkoa Rosemary Senyamule itahudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Viongoz wa ngazi ya juu waliopo madarakanii na Viongozi wastaafu.

Kumbukizi hiyo maalum itatanguliwa na ibada ya kumuombea marehemu itakayofanyika majira ya asubuhi katika uwanja huo huo wa Magufuli uliopo Chato mkoani Geita.