VITU VITATU VILIVYOMPA RAIS SAMIA UJASIRI NA UMAHIRI WA KUONGOZA NCHI BAADA YA KIFO CHA JPM

0
1424

1. MUNGU
“Mungu alitupangia mazingira mazuri ambayo tugeweza kupita salama, kwanza tumtangulize Mungu na ni yeye aliyenitia ujasiri nikaweza kwenda nalo vizuri kuongoza nchi”

2. KATIBA YETU
“La pili ni katiba yetu, katiba yetu ina miongozo ya kila kitu, inawezekana baadhi ya miongozo imepitwa na wakati yataka marekebisho lakini ina miongozo ya kila kitu, ni katiba yetu ndio iliyoelekeza itakapotokea jambo hilo Makamu wa Rais aliye madarakani atachukua nafasi na mambo yataendelea na ndio maana tumekwenda vizuri ukilinganisha na nchi nyingine ambazo katiba ipo kimya hakuna mwongozo unaosema chochote,”

3. UZOEFU
“La tatu ni uzoefu, lazima nikiri kwamba nilikuwa naye Dokta (Hayati Magufuli) tumeingia wote, tumekwenda mchaka mchaka wote, tumefanya tuliyoyafanya wote na nyinyi ni mashahidi kwamba mambo mengi hasa yanayohusu nje ya nchi alikuwa ananitanguliza mimi yeye akishughulika zaidi ndani, naweza kusema kwamba kama alinitayarisha vile alinijenga kwamba chochote kikitokea kuna mtu anaweza akachukua na akaenda na nchi”

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo katika mahojiano maalum na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt.Ayub Rioba Chacha, mahojiano yanayoangazia mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita madarakani.