Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali

0
252

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali ambapo amemteua Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa mkoa wa Njombe.

Kindamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na anachukua nafasi ya Mhandisi Marwa Rubirya ambaye amestaafu.
 
Amewateua Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi na Shamsi Vuai Nahodha ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwingine aliyeteuliwa na Rais Samìa Suluhu Hassan ni Balozi na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Ernest Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari Tanzania.

Meja Jenerali John Mbungo ambaye ni Mkurugenzi Mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Meli Tanzania (MSCL).
 
Mwingine ni Peter Ulanga aliyeteuiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Nehemia Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC.

Ulanga ni Mkurugenzi Mstaafu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) na Mchechu aliwahi kutumikia Shirika la Nyumba la Taifa kwa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na anachukua nafasi ya Dkt. Maulid Banyani, ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Kindamba na Balozi Mteule Polepole wataapishwa hapo kesho saa nne asubuhi viwanja vya Ikulu, Chamwino, Dodoma.

Uteuzi huu unaanza mara moja.