Chachacha za Gucci kuuzwa milioni 1

0
5771

Kwa sasa ulimwengu wa mitindo umepatwa na msisimuko kutoka @gucci kutokana na mojawapo ya miundo yao ya kiatu cha “jelly slippers” maarufu Afrika Mashariki kwa jina la chachacha.

Kiatu hiki cha Gucci kinauzwa dola 490 za Kimarekani, ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 1.1 za kitanzania, na ni kiatu cha miaka ya 90.

Toleo la #gucci linakuja kwa rangi nyeusi, waridi na zambarau, na limepambwa kwa motifu ya chapa ya GG.

Kwa mujibu wa Gucci.com, “Tukikumbuka mitindo ya miaka ya ’90, viatu hivi vimetengenezwa kwa raba na umaliziaji wa uwazi pia ni kutokana na ‘recalling’.

Je, unaweza kununua viatu hivi vya Milioni 1.1.?