Dkt. Gwajima awapa tuzo wanawake wafanyabiashara

0
4262

Wanawake 35 wamepewa tuzo ya umahiri kwenye biashara, tuzo zilizotolewa na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara (TWCC) .

Akikabidhi tuzo hizo mkoani Dar es Salaam, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amesema, Wanawake wanaweza kufanya mambo makubwa kwenye jamii na ametaka Wanaume kuwapa nafasi pamoja na ushirikiano.

Aidha Dkt. Gwajima amekipongeza chama hicho cha Wafanyabiashara Wanawake kwa kuandaa tuzo hizo na amekitaka mwaka ujao kiongeze idadi ya tuzo hizo na kufika 150 ili kuendelea kuwapa moyo Wanawake kufanya vizuri zaidi kwenye sekta ya biashara.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TWCC, Mwajuma Hamza amesema mchakato wa kuwapata washindi hao ulijumuisha majaji watano kutoka taasisi mbalimbali ambao walichuja majina ya Wafanyabiashara hao kwenye sekta 16 zilizokuwa zikishindaniwa kwa kuangalia vigezo vya uendelevu wa biashara husika, biashara iwe imerasimishwa na yenye nembo ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na umiliki wa biashara husika.

Tuzo hizo zimetolewa baada ya maonesho ya wiki moja ya wajasiriamali Wanawake yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kwa kushirikiana na Trade Mark East Africa pamoja na benki za CRDB, NMB na NBC.

Jumla ya wanawake 35 wamepewa tuzo ya umahiri kwenye biashara zilizotolewa na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara (TWCC) .

Wakikabidhiwa tuzo hizo mkoani Dar es Salaam na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema wanawake wanaweza kufanya mambo makubwa kwenye jamii na aliwataka wanaume kuwapa nafasi ya kwenda kufanyabiashara.

Aidha Dkt. Gwajima amekipongeza chama cha wafanyabiashara wanawake (TWCC), kwa kuandaa tuzo hizo na amewataka mwakani waongeze idadi ya tuzo hizo na kufika 150 ili kuendelea kuwapa moyo wanawake kufanya vizuri zaidi kwenye sekta ya biashara.

Mtendaji Mkuu wa (TWCC), Mwajuma Hamza amesema mchakato wa kuwapata washindi hao ulijumuisha majaji watano kutoka taasisi mbalimbali ambao walichuja majina ya wafanyabiashara hao kwenye sekta 16 zilizokuwa zikishindaniwa kwa kuangalia vigezo vya uendelevu wa biashara husika, biashara iwe imerasimishwa na yenye nembo ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na umiliki wa biashara husika

Tuzo hizo zimetolewa baada ya maonyesho ya wiki moja ya wajasiriamali wanawake yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja – Dar es Salaam na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kwa kushirikiana na Trade Mark East Africa, CRDB, NMB, NBC,