Waethiopia 78 wanaswa na Uhamiaji

0
247

Ofisi ya Uhamiaji mkoani Iringa inawashikilia raia 78 wa Ethiopia wasio na vibali, kwa kuingia nchini kinyume cha sheria.

Afisa Uhamiaji wa mkoa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Agnes Luziga amesema, wahamiaji hao wamekamatwa katika eneo la Kihesa – Kilolo ndani ya manispaa ya Iringa wakiwa wamepakizwa kwenye lori aina ya scania.

Raia hao wa Ethiopia wametokea nchini Kenya kupitia mpaka wa Holili na walikuwa njiani kuelekea nchini Afrika Kusini.

Watanzania wawili pia wamekamatwa kuhusiana na tukio.hilo la.kusafirisha wahamiaji.wasio.na.vibali.