Ujenzi wa barabara ya Mkange – Tungamaa – Pangani waanza

0
228

Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) umesema kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Mkange – Tungamaa – Pangani yenye urefu wa kilomita 120.8 na daraja la Pangani la mita 525 kutasaidia kufungua fursa za kiuchumi hasa katika nchi za Afrika Mashariki.

Kauli hiyo imetolewa jijini Tanga na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

Amesema mradi huo unafadhiriwa na benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kupitia dola bilioni 169.98 ‘za Kimarekani ambazo ni sawa na shilingi bilioni 390.

Katika mradi huo Tanzania imetoa shilingi bilioni 58.4 na kati ya fedha hizo shilingi bilioni 12.4 ni fidia kwa Wananchi.

Mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo ulisainiwa rasmi Machi 13 mwaka 2020 na wanaotekeleza mradi huo ni Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wa Kenya, barabara hiyo itapita Malindi – Lungalunga – Horohoro.