Wakulima nchini wametakiwa kuongeza uzalishaji wa kilimo himilivu cha zao la mtama ili kujiongezea kipato Kwani kuna soko la uhakika.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na mkuu wa ofisi ndogo ya shirika la chakula la umoja wa mataifa(WFP) Neema Sitta.
Amesema zao la mtama limekua likitumika kwa chakula hususani Kwa wenye mahitaji maalumu wakiwemo pia wakimbizi ambao wanapelekewa kupitia shirika la chakula duniani.
Mpaka sasa shirika la chakula duniani hapa nchini limeweza kuwasaidia wakulima kuuza mtama na kujipatia sh 13.5 bilioni mwaka 2020/21 .
Amesema wakulima wa mkoa Dodoma wameuza tani 28,000 na bado kuna soko kubwa ndani na nje ya nchi.