Serikali yashauriwa kutumia Madini kukuza uchumi

0
202

Serikali yashauriwa kutumia madini kama nyenzo ya kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuyaongezea thamani na kuyahifadhi benki.

Wito huo umetolewa mkoani Dar es Salaam na Mjumbe wa Bodi ya PADO (Asasi ya kiraia inayojishughulisha na uchambuzi wa sera na kufanya tafiti mbalimbali kwenye sekta ya madini), wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema serikali imefanikiwa kuboresha miondombinu ya biashara ya madini hivyo ni vema wakatumia fursa hiyo kuimarisha uchumi wa nchi.

Aidha Mbene ameshauri tafiti za kitaalamu zifanyike kubaini kama inawezekana kupasua miamba yenye madini bila kutumia kemikali zinazotumika hivi sasa ili kutoathiri mazingira na kuimarisha afya na uchumi wa watanzania kwa uwiano mzuri.