Kituo cha Pamoja cha Pwani chamkosha Bashungwa

0
160

Waziri wa nchi ofisi ya Rais , TAMISEMI Innocent Bashungwa amefurahishwa na Kituo cha Huduma za Pamoja ( One Stop Center) kilichoanzishwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kutoa huduma za haraka kwa Wananchi wa Mkoa huo.

Akizungumza akiwa ziarani Mkoani Pwani Bashungwa amesema uwepo Huduma muhimu sehemu moja unamrahishia mwananchi kutohangaika kuzunguka mji mzima kutafuta Ofisi mbalimbali za kutatua shida zake.

“Katika kituo hiki tunaona huduma mbalimbali zinapatikana katika eneo moja hapa tunawaona TRA, Uhamiaji, DAWASA, Magereza,TANROAD,TARURA na wengine wengi sasa mwananchi wetu wanaweza kumaliza shida zao sehemu moja na sio ile mtu anafunga safari mpaka Ofisi flani kisha unaambiwa suala hili sio la hapa nenda Ofisi nyingine inachosha lakini kwa hapa mahitaji mengi ya wananchi yanatatuliwa sehemu moja” amesema Bashungwa.

Sasa Niwatake Wakuu wa Mikoa Mingine yote nchini kuiga mfano huu na muanzishe One Stop center kwenye Ofisi zenu ili wananchi wa maeneo yenu waweze kupata huduma bora kwa urahisi na sio kusumbuka kama zamani.

Kituo cha Huduma za Pamoja Mkoani Pwani kimeanza takribani mwezi mmoja sasa na kinajumuisha Taasisi zote Wezeshi kutoka huduma katika eneo moja