Vikwazo Vikali dhidi ya Urusi kuanza leo

0
613

Waziri mdogo wa Mambo ya Nje wa Uingereza, James Cleverly, amelliambia shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Kuwa Uingereza inaleta vikwazo vikali zaidi kuwahi kutokea dhidi ya Urusi.

Vikwazo hivyo vitaanza leo na vingine zaidi vitatangazwa siku za usoni.

Amesema vikwazo hivi ni vikwazo vikali na vigumu zaidi kuliko vikwazo vyote Urusi imewahi kusikia.

Pia amesema leo asubuhi kuwa Uingereza ipo pamoja na Wananchi wa Ukraine na Uingereza itatoa msaada wa moja kwa moja kwa wananchi hao.