Ukraine imesema kwamba magari ya kivita ya Urusi yamevuka mpaka na kuingia nchini humo kutoka kona zote za taifa hilo kuanzia Belarus upande wa kaskazini mpaka Crimea upande wa kusini.
Pia wamevuka kutoka maeneo mengine ya mashariki kutoka mikoa ya Khatkiv na Luhansk.
Kulingana na vikosi vya Ulinzi, Urusi ilishambulia kwa risasi za moto kabla ya kuvuka mpaka na kuingia nchini humo.
Katika tathmini ya kijasusi ya nchi za magharibi siku 10 zilizopita, ilikadiriwa kwamba kwa Urusi kuishambulia Ukraine kwa mafanikio, kutoka kaskazini, sehemu yenye nguvu kijeshi basi wangepaswa kushambulia kutoka pande zote.
Ushuhuda wa sasa inaonyesha kwamba Urusi wanashambulia taifa hilo kutoka pande zote.
Rais wa tume ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen amesema kwamba Vladimir Putin amerudisha vita Katika bara la Ulaya.