Rais Samia: Chuo Cha elimu ya Uongozi kusaidia kuhifadhi falsafa za waasisi
Rais Samia Suluhu Hassan, amewahimiza wanasiasa na viongozi wa umoja wa vyama rafiki kujiunga na Chuo Cha elimu ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere ili kujua namna ya kutunza falsafa za waasisi wa mataifa ya vyama hivyo.
Rais Samia amesema hayo mara baada ya kufungua shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha mkoani Pwani nankuhutubia maelfu waliojitokeza kwenye sherehe hizo.
Aidha Rais Samia ameeleza umuhimu wa shule hiyo kwa vijana wanaotarajia kuwa viongozi kwa nafasi mbalimbali za Kiserikali na vyama vya Siasa wakiwa na elimu ya uzalendo na maadili kwa mataifa yao.
“Kuna vitabu vinaandikwa kuonesha kuwa nchi zetu hazifanikiwi kwa sababu ya mifumo ya Uongozi, lakini Chuo hiki kitajibu hoja zao. Chuo hiki kitabadili mitazamo ya wengi na kuzalisha wazalendo wengi wa mataifa yao” amesema Rais Samia.
Rais Samia amewasihi wasimamizi wa Chuo hicho kukisimamia kwa weledi na kukitunza ili kidumu ili kinufaisha viongozi wa sasa na WA baadaye watakaopita kusoma Chuo hicho.
Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere imejengwa kwa ushirikiano wa vyama vya Siasa vya (CPC) China, (CCM) Tanzania, (ANC) Afrika Kusini, (FRELIMO) Msumbiji, (SWAPO) Namibia, (ZANU-PF) Zimbabwe na MPLA Angola.