Biashara United yafuta uteja kwa Azam FC

0
1996

Askari wa Mpakani (Biashara United FC) imetakata katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza baada ya kuiadhibu Wanalamba lamba wa Chamazi, Azam FC kwa magoli 2-0.

Kwa ushindi huo Biashara imepanda hadi nafasi ya 12 ikiwa na alama 15, huku Azam FC imebaki katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 24.

Katika michezo mitano iliyopita kabla ya mchezo wa leo, Azam imeshinda michezo mitatu, huku zikienda sare mara mbili. Hivyo, kwa ushindi wa leo, Biashara United inakuwa imefuta uteja.

Timu hizo zitarudiana tena Juni 19 mwaka huu katika Uwanja Azam Complex mkoani Dar es Salaam.