Maofisa saba wa Polisi mkoani Mtwara wanaotuhumiwa kufanya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis (25) wamefikishwa katika mahakama ya wilaya mkoani Mtwara kwa ajili ya kesi yao kutajwa.
Waliofikishwa mahakamani leo ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje,(aliyekuwa OC-CID),Wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango,(aliyekuwa OCS) kituo cha Polisi Mtwara, Mrakibu wa Polisi Msaidizi Nicholaus Kisinza (aliyekuwa Mkuu wa Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara), Mkaguzi wa Polisi John Msuya (Aliyekuwa Mganga Mkuu Zahanati ya Polisi Mtwara), Mkaguzi wa Polisi Msaidizi Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi March 8 mwaka huu.