Serikali kuwezesha sekta binafsi

0
143

Naibu waziri wa uwekezaji viwanda na biashara na Exaud Kigahe amesema serikali it aendelee kuweka mazingira bora na wezeshi ya miundombinu ili kusaidia sekta binafsi kuzalisha bidhaa bora , shindani na nafuu ili ziweze kuongeza tija katika bidhaa zinazolishwa na ziweze kushindana vyema katika soko huru la Afrika .

Ameyaeleza hayo jijini Dar es salaam, wakati akifungua warsha ya siku siku tatu inayolenga kuongeza uwezo na uelewa kwa wafanyabishara juu ya mkataba uliosainiwa na kuridhiwa na Serikali kushiriki katika soko huru la nanma linavyojoendesha

Akizungumza katika warsha hiyo exaud amewakumbusha wafanyabiashara kuhukikisha wanaongeza ubunifu ili waweze kushiriki katika soko hilo kikamilifu.

Kwa upande wake Mwakilishi wa sekta binafsi Andrew Mahiga na Mwakilishi toka sekretariati ya soko huru la AFrica Dkt Halima Noor wamesema ni vyema wafanyabiashara wakaelewa vizuri kanuni za uendeshaji wa biashara ndani ya soko hilo kutokana na makubaliano ya Mkataba huo

Takribani nchi 55 za Afrika zenye pato ghafi la dola trilioni 3.4 zimeridhia kushiriki katika soko hilo huku zikikadiriwa kuchangia asilimia 2.5 la pato la dunia pale litakapo anza kujiendesha