Wabunge 19 wa CHADEMA ni halali

0
210

Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema kwamba wabunge 19 wa viti maaalum wa CHADEMA wapo bungeni kihalali.

Amesema hayo katika mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari bungeni jijini Dodoma.

Ameeleza kwamba kuna masharti ya mbunge kuwa ndani ya bunge, na moja wapo ni awe amedhaminiwa na chama, hivyo wabunge hao wangekuwa hawana chama wasingekuwa bungeni.

Amefafanua zaidi kwamba hatua zinazosubiriwa ni kukamilika kwa michakato inayohusu uanachama wao, na kwamba bunge likipewa taarifa rasmi kwamba wamefukuzwa, basi hawatokuwa wabunge.

Wabunge hao wa CHADEMA walifukuzwa uanachama na chama chao, lakini walikata rufaa kupinga uamuzi huo, na maamuzi ya rufaa yao bado hayajatolewa.