Dar es Salaam Jiji la sita kwa usafi Afrika

0
290

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, amesema kwa mujibu wa jarida la Tour Africa, Dar es Salaam ni jiji la sita kwa usafi katika majiji ya Afrika .

Dkt. Mpango amesema hayo katika uzinduzi wa sera ya Taifa ya mazingira ya mwaka 2021, iliyofanyika mkoani Dodoma yenye kauli mbili ‘Mimi natekeleza Sera ya Taifa ya Mazingira’.

Pia Dkt. Mpango ametumia nafasi hiyo kupongeza Manispaa ya Moshi na Iringa, kwa kuwa vinara wa usafi nchini, huku akisisitiza kazi ya kuhifadhi mazingira ikiwemo kulinda vyanzo vya maji, misitu, upandaji miti, kupendezesha miji na kufanya usafi katika maeneo ya makazi, masoko na kwenye taasisi mbalimbali ni lazima ziwe za kudumu.