Raia wa Marekani Joe Biden amewataka raia wote wa Marekani waliobaki nchini Ukraine kuondoka nchini humo mara moja, kutokana na vitisho vinavyoongezeka vya nchi ya Urusi.
Rais Biden amesema hatatuma vikosi kuwaokoa raia hao kama Urusi itavamia nchi hiyo ya Ukraine.
Amesema hali inaweza kuharibika kwa haraka sana katika eneo hilo.
Urusi mara zote imekuwa ikikana kutaka kuivamia Ukraine hata baada ya kupeleka vikosi karibia 100,000 karibu na mpaka.
Waziri mkuu wa Uingereza alisema siku ya Alhamis kuwa bara la Ulaya linakabiliana na tatizo zito la usalama baada ya miongo mingi kutokana na mvutano huu.