Zungu, mgombea pekee nafasi ya Naibu Spika wa Bunge

0
242

Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihamba amesema kuwa Mussa Zungu ndiye mgombea pekee wa nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika taarifa yake, Nenelwa amesema hadi kukamilika kwa zoezi la uteuzi wa wagombea leo saa 10:00 jioni, ni chama kimoja tu, Chama cha Mapinduzi (CCM), ndicho kilikuwa kimewasilisha jina la mgombea.

Hivyo, Februari 11, 2022 mara baada ya kipindi cha maswali na majibu, katibu atawasilisha jina la mgombea huyo mbele ya wapiga kura (Wabunge) kwa utaratibu wa uchaguzi.

Zungu anagombea nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Dkt. Tulia Ackson ambaye alijiuzulu Januari 31, 2022 ili kukidhi vigezo vya kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania.