Serikali kuwachukulia hatua wanaopandisha bei za bidhaa

0
189

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara wanaopandisha bei za bidhaa kwa makusudi.

Amesema hayo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge aliyetaka kufahamu sababu za bei za bidhaa kupanda kiholela, na serikali imejipangaje kudhibiti hali hiyo.

Amesema kuwa malighafi za bidhaa nyingi zinazotengenezwa nchini, zinapatikana hapa chini, hivyo hakuna sababu ya bidhaa kupanda bei kiholela na kwa kiasi kikubwa.

Ameongeza kwamba kama alivyosema Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Dkt. Ashatu Kijaji kwamba uchunguzi utafanyika kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa, kuangalia uwiano kati ya uwezo wake kuzalisha, na kuona kinachozalishwa, ili kujua kama kuna kampuni zinazalisha kwa kiasi kidogo ili bei ya bidhaa ipande.