Bilioni 2.4 kuboresha makumbusho ya Taifa

0
169

Makumbusho ya Taifa nchini imepatiwa shilingi Bilioni 2.4 ili iweze kutekeleza miradi 15 inayotekelezwa kwa fedha za Miradi ya Ustawu wa Nchi na Mapambano dhidi ya UVIKO 19, katika vituo vyake sita kikiwepo cha Azimio la Arusha Jijini Arusha.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga wakati akizindua Mradi mkubwa wa maboresho ya kituo cha Makumbusho ya Azimio la Arusha na Makumbusho ya Elimu Viumbe inayotekelezwa chini ya mpango wa Miradi ya Ustawi wa Nchi na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.

“Makumbusho ya Taifa ni moja ya Taasisi iliyoathirika sana kimapato kutokana na ugonjwa wa korona ambapo kumekuwa na upungufu mkubwa wa watalii wa ndani na nje ya nchi na kuathiri mapato ya Taasisi hii hivyo tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kupitia viongozi wa Wizara yetu ya Maliasili na Utalii kwa kuipatia fedha Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kutekeleza miradi katika vituo sita na maeneo ya malikale sita”. Dkt Lwoga

Dkt. Lwoga aliongeza kwa kuutaka uongozi wa vituo vyote vya Makumbusho ya Taifa nchini kuhakikisha unasimaia vyema fedha za mirahi hiyo 15 ili zilete mabadiliko yanayokusudiwa na wahakikishe miradi hiyo inakamilika kwa wakati uliopangwa.